Sound Ya Bufa episode 1

ToXic Fuvu

Wote tulivyozaliwa tulikatwa vitovu...
So nsije nikaambiwa kuna mrembo hana Kovu....
Wanaopata UKIMWI si kwamba hawajasoma shule....
Shida Condom inauzwa alafu ARV Bure....
Hata Ngono inayofanya tuzaliane ndo inatuua wazee wanafia gest...
Kutwa mada kesi...
Na ndo ubaya ukiwa nacash...
Utalea mtoto ambaye hamufanani DNA test...

Ka Mi sio mtoto wa askali ila najua kushika mtutu...
Nikiskia hela nnachojua kutoa roho ya mtu.....
Nizingue nkukokie mguu wa kuku....
Me sijuagi kurusha ngumi hayo mambo ya Makwinyo na Twaha kiduku...

Bro hi ni Bongo sio ulaya...
Sasa force love bite kwa mademu wa buza wakupige meno ka vempaya...
Na dawa ya fire si fire...
So ili hata demu kumpata ukiwa na sura mbaya itabidi uwe na hela mbaya....

Kweli jua limekua kali.....
Mpaka kuna wasanii kazi yao kujisifu tu wanajua ili tuwaite wakali...
Na ndo ujinga wa pisi kali...
Kutugaga mizinga kama nyuki ila cha ajabu wagumu kutoa asali...

Mungu ndo huruzuku si wanyonge....
Kinachokukondeshan ndo chafanya niwe bonge....
Cha msingi usione donge.....
Ata Piere kawa staa kwa ulevi wakati kuna wasanii wamepotea kwenye game kisa pombe.....

ukijikuta mtata me mwenyewe ndo mwendazimu...
We Ukinizimia data me nakuzimia Simu....
Unavimba kisa teyari umeshafika main stream....
Usijisahaulishe wasanii pia huhit kwa msimu....

Mke mwema alikuwepo ile enzi ya kambalage.....
Sikuhizi umebakia mchezo tu wa jaza nikujaze....
Kuhusu ndoa msiwaze...
Tunachezea wanaojua kubandika kucha tunaoa wanaojua kubandika maharage....

Hatupendwi na wote.....
Coz wapo wanaotaka utoke kimaisha na wapo wanaotaka maisha ya kutoke.....
Ukiwa hai unajifunza....
Hakuna anayekufa na kurudi na ndomana hakuna sanda ya mtumba.....

Nikikupa hela haimaanishi ni mzuri kupindukia...
Huenda kwenye list ya mademu zangu unashika mkia....
Hata uchafu unacost my dear....
Unaweza ukala bure afu ukaenda kunya kwenye choo cha kulipia...

Wanaovaa nguo Mpya ni watoto wa osterbay......
Wajuba nguo ikituruka tunaishusha kata kei....
amini kuwa unavuna unachopanda......
Mjamzito hula udongo na ndomana huwa anazaa mtoto mchanga.....

Curiosidades sobre la música Sound Ya Bufa episode 1 del Toxic

¿Quién compuso la canción “Sound Ya Bufa episode 1” de Toxic?
La canción “Sound Ya Bufa episode 1” de Toxic fue compuesta por ToXic Fuvu.

Músicas más populares de Toxic

Otros artistas de Heavy metal music