Dunia

Nikifikiria dunia huwaga sipati jibu
Nawaza mpaka nadata
Nikikuuliza nini dunia huwezi kunipa jibu
Hapo ndo napata utata

Mmmh muda mwingine unaweza dhani ni utani
Mbona vitu vizuri vyote viwe ni vya shetani
Eti mziki shetani, pesa nazo shetani
Mpira na pombe shetani
Mademu na mihadarati, shetani

Naamini Mungu yupo najua
Ndo ananifanya ninapumua
Akitaka hata sasa ananichukua
Ila mi nataka kujua

Ni nini dunia
Dunia dunia
Hivi ni nini dunia
Dunia eeh

Mmmh wanaoishi kwa imani
Misikitini makanisani
Uwepo wao hauonekani
Hali zao zipo taabani

Hivi ulikuaga wapi before
Hujaja duniani
Na kwanini kunakifo
Unapokwenda hapajulikani

Sawa safari ni yetu sote
Na hakuna aliyekwenda na akarudi
Japo kutusimulia
Kama pazuri ama pabaya

Uwe tajiri ama masikini
Kwa mchanga utarudi
Minatoa wosia
Tusiishi kwa ubaya

Kunakidude kinaitwa mapenzi
Hakijawahi kueleweka
Wakati wewe unalia
Mwenzako yeye anacheka

Hivi ni nini dunia
Dunia dunia
Ni nini dunia
Dunia eeh

Eeh Pedezye Kumbuka
Msalimia mwijaku

Tuombeane mwisho mwema (eeh eeh yeah)
Tuombeane mwisho mwema (maana hakuna anaejua kesho)
Tuombeane mwisho mwema (kama wewe muislamu)
Tuombeane mwisho mwema (omba kwa dini yako)
Tuombeane mwisho mwema (kama wewe ni mkristo)
Tuombeane mwisho mwema (nisiri nisiri)
Tuombeane mwisho mwema (tuombeane nisiri)

Ni nini dunia
Dunia dunia
Hivi ni nini dunia

Músicas más populares de Harmonize

Otros artistas de Afrobeats